Nafasi za Kazi Shirika la Huduma za Maktaba

Maelezo

Chanzo: Utumishi ZanzibarTarehe Iliyotolewa: 2018-07-12Kituo cha Kazi/Tukio: Zanzibar
Imetembelewa mara! 17156 ... Deadline: 2018-07-17 15:31:00

Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi katika Shirika la Huduma za Maktaba kama ifuatavyo:-

1. Mkutubi Msaidizi Daraja la III “Nafasi 2” - Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya ‘Ukutubi’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

2. Dereva Daraja la III “Nafasi 1” - Unguja 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na kupata Mafunzo ya Udereva.
• Awe na leseni hai ya Udereva kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Jinsi ya Kuomba:
• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 -ZANZIBAR.

• Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba. Muombaji anatakiwa aiainishe nafasi ya kazi anayoiomba kati ya zilizotajwa hapo juu vinginevyo maombi yake hayatazingatiwa. 

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 17 Julai, 2018 wakati wa saa za kazi.Share via Whatsapp
Advertise with us

©2024 Zenji Shoppazz . Haki zote zimehifadhiwa | Imetengenezwa na W3layouts and Zenji Shoppazz Chagua lugha : English