Nafasi za Kazi Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar

Maelezo

Chanzo: Utumishi ZanzibarTarehe Iliyotolewa: 2018-11-28Kituo cha Kazi/Tukio: Zanzibar
Imetembelewa mara! 15523 ... Deadline: 2018-12-04 15:30:00

Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kama ifuatavyo:-

1. Dereva Daraja la III “Nafasi 5”
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na kupata Cheti cha Udereva kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
• Awe na leseni hai ya udereva iliyotolewa Zanzibar.

2. Katibu Muhtasi Daraja la III “ Nafasi 3”
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Stashahada katika fani ya Uhazili kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

3. Afisa Manunuzi Daraja la II Nafasi 2”
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya Ununuzi na Ugavi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.


Jinsi ya Kuomba:
• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.

• Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 04 Disemba, 2018 wakati wa saa za kazi.Share via Whatsapp

Advertise a product

©2022 Zenji Shoppazz . Haki zote zimehifadhiwa | Imetengenezwa na W3layouts and Zenji Shoppazz Chagua lugha : English