Nafasi za kazi katika Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi

Maelezo

Chanzo: Utumishi Zanzibar



Tarehe Iliyotolewa: 2019-04-08



Kituo cha Kazi/Tukio: Zanzibar
Imetembelewa mara! 16409 ... Deadline: 2019-04-12 15:30:00

Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi katika Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kama ifuatavyo:- 

1. Mpishi Mkuu Daraja la II “Nafasi 1” Unguja 

Sifa za Waombaji: 
•Awe ni Mzanzibari. 
•Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Ukarimu na Usimamizi wa Mambo ya Utalii na Uzoefu wa kazi ya Upishi usiopunguwa miaka (8) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 



2.Msaidizi Mpishi Mkuu Daraja la III “Nafasi 1” Unguja 

Sifa za Waombaji: 
•Awe ni Mzanzibari. 
•Awe amehitimu elimu ya Stashahada katika fani ya Ukarimu na Usimamizi wa Mambo ya Utalii na Uzoefu wa kazi ya Upishi usiopunguwa miaka (5) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 


3.Wapishi Daraja la III “Nafasi 2” Unguja na 2” Pemba 

Sifa za Waombaji: 
•Awe ni Mzanzibari. 
•Awe amehitimu elimu ya Stashahada katika fani ya Ukarimu na Usimamizi wa Mambo ya Utalii kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 



4.Wahudumu Daraja la III “Nafasi 4” Unguja na 6” Pemba 

Sifa za Waombaji: 
•Awe ni Mzanzibari. 
•Awe amemaliza elimu ya Sekondari. 



5.Fundi Magari Daraja la III “Nafasi 1” Unguja 


Sifa za Waombaji: 
•Awe ni Mzanzibari. 
•Awe amehitimu elimu ya Cheti katika fani ya Ufundi Magari kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 




Jinsi ya Kuomba: 
•Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:- 



KATIBU, 
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI, 
S. L. P 1587 - ZANZIBAR. 

•Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba. Muombaji anatakiwa kuainisha nafasi anayoiomba vyenginevyo maombi yake hayatazingatiwa. 

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:- 
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo 
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari) 
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa. 
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari. 
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni. 
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa. 
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 12 Aprili, 2019 wakati wa saa za kazi. 



Share via Whatsapp
Advertise with us

©2024 Zenji Shoppazz . Haki zote zimehifadhiwa | Imetengenezwa na W3layouts and Zenji Shoppazz Chagua lugha : English