Nafasi za kazi ya Ualimu Kaskazini A

Maelezo

Chanzo: Utumishi ZanzibarTarehe Iliyotolewa: 2019-04-08Kituo cha Kazi/Tukio: Zanzibar
Imetembelewa mara! 20261 ... Deadline: 2019-04-12 15:30:00

Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi ya Ualimu kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini ‘A’ kwa Skuli ya Msingi ya Banda Maji, Chutama, Chaani, Fukuchani, Gamba, Jongowe, Kibeni, Kibuyuni, Kidagoni, Kidoti, Kilimani, Kilindi, Kinyasini, Kivunge, Mfurumatonga, Mkokotoni, Mkwajuni, Moga, Mto Pwani, Nungwi, Pale, Potoa, Tumbatu na Pwani Mchangani kama ifuatavyo:-


1.Walimu wa Cheti Sanaa nafasi 19
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe na elimu ya Cheti cha Ualimu cha Sanaa kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
2.Walimu wa Cheti Sayansi Nafasi 14
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe na elimu ya Cheti cha Ualimu wa Sayansi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
3.Walimu wa Diploma ya Msingi Sanaa Nafasi 9
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe na elimu ya Stashahada ya Ualimu wa Sanaa kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
4.Walimu wa Diploma ya Msingi Sayansi Nafasi 17
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe na elimu ya Stashahada ya Ualimu wa Sayansi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Jinsi ya Kuomba:
•Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU, TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587, 
ZANZIBAR.•Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba. Muombaji anatakiwa kuainisha nafasi pamoja na Skuli anayoiomba vyenginevyo maombi yake hayatazingatiwa.Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo 
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 12 Aprili, 2019 wakati wa saa za kazi.

•Tangazo hili pia linapatikana katika Tovuti www.utumishismz.go.tzShare via Whatsapp
Advertise with us

©2024 Zenji Shoppazz . Haki zote zimehifadhiwa | Imetengenezwa na W3layouts and Zenji Shoppazz Chagua lugha : English