Nafasi za kazi kada mbali mbali kwa ajili ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idar

Maelezo

Chanzo: Utumishi Zanzibar



Tarehe Iliyotolewa: 2019-04-18



Kituo cha Kazi/Tukio: Zanzibar
Imetembelewa mara! 13101 ... Deadline: 2019-04-25 15:30:00

Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi katika kada mbali mbali kwa ajili ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ kama ifuatavyo:-



BARAZA LA MJI WETE PEMBA (Nafasi 9)

1.Mlinzi Daraja la III “Nafasi 1”

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na kupata Mafunzo ya Ulinzi kutoka JKU au JKT.



2.Wasafishaji Mji Daraja la III “Nafasi 3” 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na kufaulu.



3.Walimu wa Stashahada ya Sanaa “Nafasi 5”
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe na elimu ya Stashahada ya Ualimu wa Sanaa kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar



BARAZA LA MJI MKOANI PEMBA (Nafasi 13)



1.Wasafishaji Mji Daraja la III “Nafasi 5” 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na kufaulu.



2.Walimu wa Stashahada ya Sanaa “Nafasi 8”

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe na elimu ya Stashahada ya Ualimu wa Sanaa kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar



BARAZA LA MJI CHAKE CHAKE PEMBA (Nafasi 37)

1.Walimu wa Cheti Msingi “Nafasi 25” kwa ajili ya Skuli za Shungi, Kwale, Madungu, Ng’ambwa, Ole, Uwandani,Chanjamjawiri, Chanjaani, Pujini, Michakaeni, Wawi, Kilindi, Pembeni na Ziwani.
Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe na elimu ya Stashahada ya Ualimu wa Sanaa kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar



2.Wahudumu Daraja la III “Nafasi 5” 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe na elimu ya Sekondari na kufaulu

3Wauguzi Daraja la III “Nafasi 2” 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Uuguzi (Diploma in Nursing) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.



4Afisa Kilimo Msaidizi Daraja la III “Nafasi 1” 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu elimu ya Stashahada katika fani ya Kilimo kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.



5Bwana/Bibi Shamba Daraja la III Nafasi 1” 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu elimu ya Stashahada katika fani ya Kilimo kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.



6Karani Diko Daraja la III “Nafasi 1”

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu elimu ya Sekondari na kufaulu.



7Mlinzi Daraja la III “Nafasi 1”


Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na kupata Mafunzo ya Ulinzi kutoka JKU au JKT.



8Afisa Maabara Daraja la III “Nafasi 1 ” 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Maabara kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 





MKOA WA KUSINI UNGUJA 

1.Dereva Daraja la III “Nafasi 1” 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na kupata Cheti cha Udereva.
•Awe na leseni hai kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.



HALMASHAURI YA WILAYA YA KATI UNGUJA


1.Afisa Uendeshaji Msaidizi Daraja la III “Nafasi 1” 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Stashahahada katika fani ya Utawala wa Umma au Rasilimali watu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar



2.Walimu wa Skuli za Msingi “Nafasi 8” kwa ajili ya Skuli za Kidimni, Marumbi, Mwera, Bambi, Ukongoroni, Unguja Ukuu

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe na elimu ya Stashahada ya Ualimu wa Sanaa kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar



3.Msaidizi Afisa Takwimu Daraja la III “Nafasi 1” 


Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu elimu ya Stashahada katika fani ya Takwimu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar



WILAYA YA KUSINI UNGUJA



1.Fundi Bomba Daraja la III “Nafasi 1” 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Cheti au stashahada katika fani ya Ufundi Bomba kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

2.Tarishi Daraja la III “Nafasi 1 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na kufaulu.




WILAYA YA KATI UNGUJA

1.Mwandishi wa Habari Daraja la III “Nafasi 1”

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu elimu ya Stashahada katika fani ya Uandishi wa Habari kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar


2.Mlinzi Daraja la III “Nafasi 1 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na kupata mafunzo ya Ulinzi kutoka JKU au JKT.


Jinsi ya Kuomba:
•Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-



KATIBU, TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587, 
ZANZIBAR.

•Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba. Muombaji anatakiwa kuainisha nafasi ya kazi pamoja na Skuli anayoiomba vyenginevyo maombi yake hayatazingatiwa.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo 
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
g)Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 25 Aprili, 2019 wakati wa saa za kazi.



Share via Whatsapp
Advertise with us

©2024 Zenji Shoppazz . Haki zote zimehifadhiwa | Imetengenezwa na W3layouts and Zenji Shoppazz Chagua lugha : English