Nafasi za Kazi MKURABITA (Re-advertised)

Maelezo

Chanzo: Utumishi TanzaniaTarehe Iliyotolewa: 2019-05-18


Download


Kituo cha Kazi/Tukio: Tanzania
Imetembelewa mara! 23145 ... Deadline: 2019-05-30 15:30:00

TANGAZO LA NAFASI YA KAZI (LINARUDIWA) 
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Mpango wa 
Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) 
anakaribisha maombi kutoka kwa Watanzania wenye sifa wa kujaza nafasi moja (1) ya 
kazi kama ilivyoainishwa kwenye tangazo hili. 
1.0 MPANGO WA KURASIMISHA RASILIMALI NA BIASHARA ZA WANYONGE 
TANZANIA (MKURABITA) 
Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania maarufu kama “MKURABITA” ni miongoni mwa jitihada za Serikali katika kuwezesha jamii kiuchumi. MKURABITA imeanzishwa na Serikali ya Tanzania mwaka 2004 kwa lengo la kuwapa nguvu ya kiuchumi wananchi kwa kuwaongezea uwezo wa kumiliki na kufanya biashara katika mfumo rasmi unaozingatia utawala wa Sheria. Mpango huu unasimamiwa na kuratibiwa na Ofisi ya Rais, Ikulu. 
MKURABITA ni sehemu ya Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Tanzania (MKUKUTA) na Mkakati wa Kuondoa Umasikini Zanzibar (MKUZA), ukilenga kuwawezesha walengwa kutumia rasilimali na biashara zao zilizorasimishwa katika kujipatia mitaji, soko pana na fursa zingine zinazopatikana katika sekta rasmi na hivyo kupunguza umaskini wa kipato. 

 

PLEASE DOWNLOAD PDF FILE HERE FOR MORE INFORMATION

 Download

Share via Whatsapp
Advertise with us

©2024 Zenji Shoppazz . Haki zote zimehifadhiwa | Imetengenezwa na W3layouts and Zenji Shoppazz Chagua lugha : English