Nafasi za kazi Mamlaka ya Hifadhi na Uendelezaji Mji Mkongwe

Maelezo

Chanzo: Utumishi ZanzibarTarehe Iliyotolewa: 2019-06-28Kituo cha Kazi/Tukio: Zanzibar
Imetembelewa mara! 24497 ... Deadline: 2019-07-05 15:30:00

Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi kwa ajili ya Mamlaka ya Hifadhi na Uendelezaji Mji Mkongwe kama ifuatavyo:-

1. Afisa Miradi Daraja la II “Nafasi 1” 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Mipango au Mipango ya Maendeleo (Regional Development Planning) au Uchumi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

2. Mwangalizi wa Ofisi Daraja la III “Nafasi 1” 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Utawala wa Umma au Rasilimali Watu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

3. Mtunza Ghala Daraja la III “Nafasi 1” 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Ununuzi na Ugavi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

4. Fundi Sermala Daraja la III “Nafasi 2” 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Sekondari na kupata Cheti cha Ufundi Seremala kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

5. Fundi Muashi Daraja la III “Nafasi 1” 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Sekondari na kupata Cheti cha Ufundi Muashi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

6. Fundi Umeme Daraja la III “Nafasi 1” 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Sekondari na kupata Cheti cha Ufundi Umeme kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar


Jinsi ya Kuomba:
• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU, 
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.

• Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba. 

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo 
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 05 Julai, 2019 wakati wa saa za kaziShare via Whatsapp

Advertise a product

©2022 Zenji Shoppazz . Haki zote zimehifadhiwa | Imetengenezwa na W3layouts and Zenji Shoppazz Chagua lugha : English