Nafasi za Kazi Afya OR-TAMISEMI

Maelezo

Chanzo: Utumishi TanzaniaTarehe Iliyotolewa: 2020-01-21


Download


Kituo cha Kazi/Tukio: Tanzania
Imetembelewa mara! 28474 ... Deadline: 2020-02-07 15:30:00

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 
OFISI YA RAIS 
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA 
TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA 
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR - TAMISEMI) kwa kushirikiana  na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Taasisi ya  Benjamin William Mkapa inatekeleza Mradi wa Kuimarisha Mifumo Stahimilivu na  
Endelevu ya Afya (RSSH) kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa kupambana na  UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria (Global Fund). 
Mradi huu una lengo la kuimarisha huduma za afya ngazi za vituo katika Mikoa kumi  (10) iliyopewa kipaumbele na mradi huu ambayo ni Mwanza, Shinyanga, Mara,  Simiyu, Geita, Kagera, Katavi, Tabora, Dodoma na Kigoma.  
Hivyo, Ofisi ya Rais - TAMISEMI kwa kushirikiana na Taasisi ya Benjamin William  Mkapa inapenda kuwatangazia wahitimu wa kada za afya nchini kuwasilisha maombi  
ya nafasi za kazi, kuanzia tarehe 20/01/2020 ili kujaza nafasi mbalimbali za Kada ya  Afya katika Hospitali za Wilaya, Vituo vya Afya na Zahanati.

 

TAFADHALI BOFYA KITUFE HAPO CHINI ILI KUDOWNLOAD PDF FILE KWA TAARIFA ZAIDI Download

Share via Whatsapp

Advertise a product

©2022 Zenji Shoppazz . Haki zote zimehifadhiwa | Imetengenezwa na W3layouts and Zenji Shoppazz Chagua lugha : English